Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Samuel Kosgei
Kituo cha radio Radio Jangwani kinaadhimisha miaka 9 tangu kuanzishwa kwake huku kikisalia kuwa nguzo muhimu kwa jamii ya wafugaji wa Marsabit kwa kutoa habari, malezi ya kiroho, na hata burudani.
Baadhi ya mashabiki wa mwanzo wa radio jangwani wakiongozwa na Isaac Leria maarufu kama Mzee Dokhle kutoka eneo la Karantina mjini Marsabit wamesema kuwa kituo hiki kimewafaa kwa kupata matangazo bomba na habari nyingi ambazo zimewaelimisha.
Anasema kuwa amepata marafiki wengi wapya kupitia radio hivyo kuomba mashabiki kuzidi kujuliana hali kupitia kituo cha jangwani.
Ali Hapicha kutoka Butiye Moyale mmoja wa mashabiki wa mwanzo hapa Jangwani amesema kuwa ujio wa radio Jangwani imefaa kwani kinafahamisha kuhusu haki za kibinadamu haswa wafugaji Marsabit.
Ameongeza pia kuwa imesaidia kuwajibisha na kusukuma viongozi kuhudumia wananchi mashinani.
Kauli yake hiyo imesisitizwa na Mama Nguvu kutoka Old Town mjini Marsabit ambaye pia ni shabiki wa kituo hiki aliyetaka wasikilizaji kuzidi kusikiza radio jangwani ili kiwe bora Zaidi.
Alkano kutoka Merile kwa upande wake amesema kuwa kituo hiki kimejali lugha zote kuu za Marsabit kwa kupeperusha matangazo kupitia lugha zao za mama.
Pia amerai uongozi wa kituo hiki kuwaandalia warsha ambayo itawaleta mashabiki wote pamoja.
Martha Kula kutoka mjini Marsabit aidha amesema kuwa maudhui ya kidini yanamfaa sana kwa kukuza na kuinua Imani ya wasikilizaji.
Akizungumza ofisini mwake, Meneja wa kituo cha Radio Jangwani, Silvio Nangori, ameeleza kuwa safari ya miaka tisa imekuwa ya mafanikio makubwa licha ya changamoto mbalimbali.
Ameahidi kuwa kama vile kauli mbiu ya kituo hiki – baragumu ya faraja inavyosema basi wasikilizaji watazidi kupata furaha na faraja kupitia vipindi na matangazo bomba.
Mkurugenzi wa kituo hiki Padre Ibrahim Racho kwenye ujumbe wake ameshukuru wasikilizaji wa radio jangwani kwa kuwa familia moja kubwa huku akiwaombea wote Baraka na Neema zake Mungu siku zote. Amesema kuwa kituo hiki kitazidi kuwa kitovu cha kueneza injili na neno la Mungu kwa wasikilizaji,.
Tangu kuanzishwa kwake tarehe 18 mwezi Machi mwaka wa 2016, redio hii inayomilikiwa na Jimbo Katoliki la Marsabit imejikita katika kueneza Injili, kuhamasisha amani, na kutoa elimu kwa jamii.