Local Bulletins

Onyo limetolewa kuhusiana na matumizi ya sigara aina ya ORIS Moyale kaunti ya Marsabit.

Na Carol Waforo

Tahadhari imetolewa kuhusiana na utumizi wa sigara aina ya ORIS haswa kwa wakaazi wa eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.

Imebainika kuwa ORIS inatumika kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo hii ikichangiwa sana na mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Ni tahadhari ambayo imetolewa na afisa wa watoto katika shirika la SND Joan Chebet baada ya kubainika kuwa pia watoto walio na chini ya umri wa miaka 18 wanaitumia.

Eneobunge hilo la Moyale linaendelea kukabiliana na kero la utumizi wa dawa za kulevya kutokana na mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Aidha amewataka jamii kushirikia na idara husika ili kufanikisha vita dhidi ya dawa hizi za kulevya.

Na huku kiangazi ikiendelea kushuhudiwa humu jimboni Marsabit afisa huyu wa watoto anasema kuwa baadhi ya watoto wanakosa kuhudhuria masomo ili kusaidia katika shughuli za kusaka maji nyumbani jambo linalowanyima watoto haki ya elimu.

Haya yanajiri huku mamlaka ya kutathmini hali ya ukame nchini NDMA ikisema kuwa wananchi milioni 2.15 kutoka maeneo kame nchini wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Kaunti zinazoathirika pakubwa na kaunti ya Marsabit Turkana, Mandera, Garissa, Wajir

Subscribe to eNewsletter