Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Carol Waforo
Onyo kali limetolewa kwa yeyote aliye na nia ya kutekeleza mashumbulizi ya wizi wa mifugo kwa nia ya kulipiza kisasi baada ya washukiwa watatu wa wizi wa mifugo kuuawa na maafisa wa polisi hivi wiki moja iliyopita.
Onyo hili limetolewa na kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau alipozungumza na wanahabari afisini mwake baada ya kufanya ziara katika eneo la mkasa ambapo mhudumu moja wa bodaboda aliuawa kinyama kwa kudungwa kisu katika eneo la Arobota nje kidogo na mji wa Marsabit.
Kamishna Kamau amesema kuwa walio na nia kama hiyo watakabiliwa vikali na mkono wa sheria.
Kadhalika ameendelea kuonya wanasiasa wanaodaiwa kusaidia wahalifu katika kutekeleza mashambulizi haya.
Watatu hao waliuawa Jumatatu ya tarehe 3 baada ya jaribio la shambuli la wizi wa mifugo kutibuka.
Katika kisa hicho maafisa wa polisi walifanikiwa kunasa bunduki 2 moja aina ya AK 47 na nyingine aina ya G3 pamoja na risasi 6.