Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
ALIYEKUWA mwaniaji wa ugavana kaunti ya Marsabit mwaka wa 2022 Pius Yattani Wario amepuuza uwepo wa maendeleo katika kaunti ya Marsabit yaliyoanzishwa na serikali ya gavana Mohamud Ali.
Wario maarufu kama Ole Woiye amesema kuwa kufikia sasa hajaona maendeleo yoyote kama alivyodai mdhibiti wa bajeti kwenye ripoti yake.
Ole Woiye amesema kuwa cha msingi kwa sasa ni wafanyakazi wa serikali kulipwa mishahara yao wanayodai serikali ya kaunti ya Marsabit.
Wakati uo huo ameunga mkono uhusiano mpya kati ya kinara wa ODM Raila Odinga na rais William Ruto akIsema kuwa ushirikiano huo utaponya umoja wa taifa haswa baada ya serikali hii kutikiswa na wimbi la maadamano tangu rais Ruto apate madaraka.