Mwanaume mmoja mweye umri wa miaka 24 afariki baada ya kugongwa na nyaya za umeme katika eneo la Dirib Gombo.
February 27, 2025
Na JB Nateleng,
Mwanaume mmoja mweye umri wa miaka 24 amefariki baada ya kugongwa na nyaya za umeme katika eneo la Dirib Gombo, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit
Akidhibitisha kisa hicho chifu wa Lokesheni ya Dirib Gombo Katelo Galgallo amesema kuwa mwanaume huyu aliaga dunia papo hapo baada ya kuguza nyaya hizo za umeme hii leo mida ya saa nne asubuhi.
Chifu Katelo amealaumu utepetevu wa kampuni ya umeme Kenya Power kwa kukosa kuboresha vikingi vya stima katika eneo hilo kwa muda sasa jambo ambalo ametaja kuwa linahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
Kwa upande wake mjomba wa mwendazake Guyo Abata amesema kuwa wamekuwa wakiripoti visa vya vikingi hivyo kuliwa na mchwa lakini kampuni ya Kenya Power haijachukua hatua hatua zozote.
Hata hivo wawili hao wametoa wito kwa kampuni ya Kenya Power kuweza kuzuru eneo hilo na kurekebisha vikingi vya stimia vilivyo na matatizo katika eneo hilo ili kuimarisha usalama wa wakaazi.