Local Bulletins

Mwanaume ashtakiwa mahakama ya Marsabit kwa kosa la kumnajisi mtoto wa miaka 8.

Mwanaume mmoja ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kumnajisi mtoto mdogo wa umri wa miaka minane.

Lmeseku Lealo mwenye umri wa makamo anadaiwa kumtendea unyama mtoto huyo mnamo tarehe 16 mwezi uliopita wa Februari katika lokesheni ya Songa, kaunti ndogo ya Marsabit ya kati, gatuzi la Marsabit.

Kulingana na mashtaka mshukiwa alikusudia alimnajisi mtoto huyo mdogo kinyume cha sheria.

Akifika mbele ya mahakama ya Marsabit hapo jana Jumatatu, mshukiwa amehoji kuwa mtoto huyo ni jamaa yake, swala ambalo hakimu mwanadamizi wa mahakama ya Marsabit, Simon Arome ameamru taarifa mpya kuandikisha kuhusu kesi hiyo.

Mahakama mnamo Februari, 18 mwaka huu, ilikuwa imemwechalia mshukiwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili pesa taslimu au mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Subscribe to eNewsletter