Local Bulletins

Mwanamme mmoja ahukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani baada ya kupatikana na kosa la kumiliki risasi 4 katika eneo la Wabera, Marsabit.

Mwanamme mmoja ahukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani baada ya kupatikana na kosa la kumiliki risasi 4 katika eneo la Wabera, Marsabit.

Na Waandishi Wetu,

Mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani katika gereza la Marsabit baada ya kupatikana na kosa la kumiliki risasi.

Mahakama iliarifiwa kuwa mnamo tarehe 5 mwezi Mei mwaka wa 2023, mshukiwa kwa jina Mohamed Mutua Hassan alipatikana na risasi nne akiwa katika boma moja eneo la Wabera viungani vya mji wa Marsabit.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi katika mahakama ya Marsabit Christine Wekesa, mshukiwa alikana mashtaka hayo huku akidai kuwa boma alikuwemo wakati wa kukamatwa kwake hakukuwa nyumbani kwake ila ni nyumbani kwa babake ambaye tayari ameshaanga dunia.

Upande wa mashtaka ulidhibitisha kwamba mshukiwa alimiki risasi hizo wakati wa kukamtwa kwake.

Aidha mshukiwa alijejetea kwamba pia ana watoto wachanga ambao wanamtegemea.

Ana 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Subscribe to eNewsletter