Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na JB Nateleng,
Eneo la Loiyangalani linahitaji zaidi ya walimu 12 wa chekechea (ECDE) ili kuimarisha elimu katika eneo hilo.
Haya yamebainika katika kongamano lililowaleta pamoja washikadau wa elimu jimboni Marsabit pamoja na wawakilishi wadi, ililofadhiliwa na shirika la World Vision.
Kwa mujibu wa mwakilishi wadi wa Loiyangalani Daniel Emojo ni kwamba walimu 12 wanahitajika ili kuinua hadhi ya elimu katika eneo la Loiyangalani kwani shule nyingi za chekechea katika eneo hilo zinauhaba wa walimu.
Mwakilishi wadi huyo ameichangamoto idara ya elimu jimboni kuwaajiri walimu waliohitinu na ambao bado hawajapata ajira kwa TSC ili kutatu changamoto hiyo ya uhaba wa waalimu.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu kaunti ya Marsabit Ambaro Abdulah Ali ni kwamba watawatumia wanafunzi wa nyanjani (Interns) ambao wamekuwa wakihudumu katika shule tofauti eneo la Loiyangalani kama suluhisho la muda mfupi huku wakitarajia kuwaajiri walimu zaidi ya 100 katika mwaka ujao wa kifedha.