Local Bulletins

Mvua zinazoshuhudiwa katika kauti ya Marsabit sio za kutegemewa – Wasema wataalam.

Na Joseph Muchai,

Mvua zinazoshuhudiwa katika kauti ya Marsabit sio za kutegemewa.

Haya ni kwa mujibu wa wataalam katika kaunti ya Marsabit. Tahadhari hii imetolewa kwa wakaazi wakionywa kuwa mvua itanyesha kwa kipindi kifupi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka ya kukabiliana na kiangazi katika kaunti ya Marsabit Guyo Golicha ni kuwa huenda kukashuhudiwa kiangazi punde baada ya mvua za sasa kusita.

Aidha Golicha amewataka wafugaji kuchukua tahadhari kwani sehemu za kuhifadhia maji ya mifugo kwa sasa haziwezi kutegemewa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo muhimu.

Vile vile ameonya uwezekano wa kupanda kwa bei za bidhaa za sokoni kutokana na uhaba wa mavuno unaotarajiwa kushuhudiwa.

Sehemu zilizo kwenye hatari zaidi ya kukabiliwa na uhaba wa mvua kulingana na Golicha ni kama zifuatazo.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa jimboni Marsabit Abdi Jilo kuonya kuhusiana na uhaba wa mvua katika msimu huu.

Subscribe to eNewsletter