Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Carol Waforo
Mwanaume mmoja ameuawa na ndovu mapema leo Alhamisi katika eneo la Karare eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.
Haya yamethibitishwa na mkurungenzi msaidizi wa shirika la huduma za wanyamapori KWS ukanda wa kaskazini mashariki Bakari Chongwa ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani.
Kulingana na Chongwa bado haijabainika iwapo mhasiriwa aliuawa ndani au nje ya mbuga ya wanyapori akisema kuwa bado uchunguzi unaendelea.
Kulingana na sheria fidia hutolewa iwapo maafa yametokea ndani ya mbuga za wanyapori kama anavyoeleza Chongwa.
Vile vile wananchi humu jimboni na haswa walio karibu na mbuga za wanyapori wametakiwa kutoa taarifa kwa shirika hilo la wanyapori KWS kuhusu visa vyovyote vya mzozo kati ya wanyama na binadamu ili hatua ichukuliwe kwa haraka.