Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
NA SAMUEL KOSGEI
WAZAZI katika eneo la Lokesheni ya Namarei eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wamehimizwa kuchukua tahadhari ya wanyamapori kama vile fisi ambao siku za hivi maajuzi wameonekana wakitembea ovyo ovyo katika maeneo wanayoishi watu.
Chifu wa Namarei Andrew Lemaro akizungumza na idhaa hii amesema kuwa wazazi wanafaa kuhakikisha kuwa watoto wao wapo katika hali salama wakati wanyama wanaposaka lishe na maji kwenye manyatta za watu.
Kauli yake Chief Lemaro inajiri siku moja baada ya msichana wa miaka 12 kuvamiwa na fisi usiku alipokuwa nyumbani kwao.
Amewataka wazazi kuwa makini na waangalifu haswa watoto wao wanapochunga mifugo na hata wanapoenda shule mapema asubuhi ili kuepuka uvamizi wa fisi na wanyama wengine.
Anasema huenda kutokana na hali ya kiangazi wanyama watarandaranda sana karibu na makaazi ya watu.
Aidha ameambia Radio Jangwani kuwa kwa sasa hali ya chakula ni mbaya ikizingatiwa kuwa kwa sasa kiangazi imeongezeka kutokana na ukosefu wa mvua ya muda mrefu.
Mifugo anasema inahangaika sana kutokana na ukosefu wa lishe na maji sawa na binadamu.