Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Idara ya utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit imesema kuwa msimu wa mvua za kawaida za mwezi tatu, nne na tano bado hazijaanza.
Mkurugenzi wa idara hiyo Abdi Dokata ameambia shajara kuwa mvua zilizoshuhudiwa Marsabit na baadhi ya sehemu nchi maajuzi zilikuwa mvua za kupita tu bali msimu wa mvua za vuli haujaanza hadi mwezi wa nne.
Kwenye ripoti ya hali ya hewa ya msimu huu wa miezi mitatu ijayo idara hiyo imesema kuwa mvua chini ya wastani itashuhudiwa kote jimboni japo kwa viwango vya chini.
Dokata mwezi uliopita kwenye ripoti alisema kuwa kilele cha mvua hizo itakuwa mwezi wa nne katika kaunti hii ya Marsabit.
Eneobunge la Saku anasema kuwa itapokea mvua kiasi kuanzia wiki ya 1-2 ya mwezi wa nne sawa na kaunti ndogo ya Moyale.
Maeneobunge ya North Horr na Laisamis amesema itapokea mvua kiwango cha chini sana kuanzia wiki ya pili ya mwezi Aprili.