KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Mwandishi Wetu
MTU mmoja ameuawa na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya majambazi kuvamia kijiji kimoja nje kidogo ya mji wa dukana usiku wa kuamkia leo.
Kamishna msadizi wa divisheni ya Dukana Nazarene Njuki amedhibitisha kisa hicho akisema kuwa tayari idara ya usalama imeimarisha doria katika eneo hilo wakishirikiana na maafisa wa akiba NPR.
Amedai kuwa huenda ikiwa ni kisa cha kulipiza kisasi au ni mpango wa kuleta uhasama miongoni mwa jamii zinazoishi pande mbili za mpakani.
Huku akisema kuwa serikali inatumia mbinu mbalimbali kuleta usalama na utulivu Njuki amewarai wakaazi wa sehemu hiyo kukumbatia Amani huku serikali ikijizatiti kutuliza hali.
Shambulizi hilo linajiri wiki moja iliyopita baada ya kijana mmoja kuuliwa wiki mbili zilizopita katika eneo hilo la mpakani Dukana. Watu wengine watatu waliua pia katika eneo la Dilo Ethiopia na wengine wanne kujeruhiwa kwenye kisa kinachodaiwa kuwa cha kulipiza kisasi.
Siku ya Jumatano mkutano wa amani uliandaliwa mjini Moyale mpaka wa Kenya na Ethiopia, mkutano ambao uliwaleta pamoja washikadau kwenye idara ya usalama kutoka mataifa yote mawili.