Local Bulletins

MILA POTOVU KAMA VILE UKEKETAJI, NA NDOA ZA MAPEMA ZIMETAJWA KAMA CHANGAMOTO KUU ZIZOADHIRI ELIMU YA MTOTO WA KIKE HAPA JIMBONI MARSABIT.

NA ISAAC WAIHENYA

Mila Potovu kama vile ukeketaji, na ndoa za mapema zimetajwa kama changamoto kuu zizoadhiri elimu ya mtoto wa kike hapa jimboni Marsabit.

Kwa mujibu wa Rahma Wako mkuregenzi katika shirika shirika la Peace and Prosperity Initiative (PPI) katika kaunti ya Marsabit ni kuwa mila hizo pia huchangia mimba za utoto ambazo zinaadhiri elimu ya wasichana kwa kiwango kikubwa.

Kwenye mazungumzo na meza ya Radio Jangwani Rahma ametoa wito kwa serekali kuekeza katika kujenga vituo vya kuokoa wasichana maarufu kama kama Rescue Centers ili kuwahifadhi wasichana wanaowaokoa kutoka kwa wanaoendeleza dhulma hizo.

Ametoa wito kwa jamii kuasi kukeketa wanao kwani zoezi hilo linaadhiri maisha yao ya baadae.

Aidha Rahma pia amependekeza kujengwa kwa kituo cha kurekebishia tabia katika eneo bunge la Moyale ili kuwaokoa vijana ambao amesema kuwa kwa idadi kubwa wamepotelea kwenye utumizi wa mihadarati na dawa za kulevya kutokana na eneo hilo kuwa mpakani.

Subscribe to eNewsletter