Local Bulletins

Michezo ya mipira yaanza katika kaunti ndogo ya Saku, Marsabit

NA ABRAHAM WAWERU

Wachezaji wa mchezo wa raga katika shule za upili kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutia bidii katika mazoezi yao ili kuhakikisha matokeo bora katika michuano  ya kaunti ndogo.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani nahodha wa timu ya raga kutoka shule ya upili ya ACK St. Peters Dima Huka amesema kuwa mchezo ungali geni katika sehemu nyingi za Marsabit hivyo kuna haja ya mchezo huo kukuzwa Zaidi.

Vile vile wachezaji hao wamesema kuwa wana matarajio ya kuandikisha matokeo mazuri kwa timu zao watakaposhiriki michuano ya kaunti ndogo.

Subscribe to eNewsletter