Local Bulletins

Meneja katika afisi ya MCA akabiliwa na kosa la unajisi wa msichana wa miaka 14 Marsabit.

Na Mwandishi Wetu
Meneja katika afisi ya mwakilishi wadi wa Sagante Jaldesa Sora Duba anakabiliwa na kosa la unajisi wa msichana wa gredi ya saba wa miaka 14.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani Kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa mshukiwa huyo anadaiwa kutekeleza kitendo hicho nyumbani kwake.
Mshukiwa alikamatwa tarehe 21 mwezi Machi na kuwaachiliwa na pesa taslimu shilingi elfu 100,000 huku akitarajiwa kufikishwa mahakami siku ya hapo kesho Jumanne.
Wakati uo huo
Mwanaume moja anasakwa na maafisa wa polisi kwa madai ya kumuoa msichana chini ya umri wa miaka 18 kule katika kijiji cha Balah lokesheni ya Korr eneo bunge la Laisamis.
Mshukiwa Mundolo Machan anadaiwa kumuoa msichana wa miaka 14 na kuishi naye nyumbani kwake kati ya Januari tarehe 29 hadi Machi tarehe 27.
Kulingana na taarifa ya polisi msichana huyo alitoroka na kupiga ripoti katika kituo cha polisi.
Inadaiwa kuwa nduguye msichana huyo ndiye aliyemwoza baada yake kumlazimisha kuacha masomo akiwa gredi ya 3.
Kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema uchunguzi unaendelea kuhusiana na kisa hicho.

Subscribe to eNewsletter