Local Bulletins

Mashirika ya kijamii pamoja na wananchi katika kaunti ya Marsabit watakiwa kushirikiana ili kufanikisha mageuzi.

Na Isaac Waihenya,

Wito umetolewa kwa mashirika ya kijamii pamoja na wananchi kushirikiana ili kufanikisha mageuzi katika kauti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la Forum CIV Jackson Obare aliyezungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee baada ya hafla ya leo iliyoyaleta pamoja mashirika ya kijamii yanayofadhiliwa na shirika hilo ambayo ni HODI, IREMO, IFPC, SAF,na shirika la Isiolo Gender Watch (IGW) ni kuwa warsha hii ililenga kutoa hamasa ya kufanya kazi kwa Pamoja saw ana kusaka Suluhu la maswala yanayoadhiri wananchi wa kaunti ya marsabit yakiwemo ukosefu wa usalama,mizozo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la IREMO Mwalimu Lokho Abduba nae amekariri haja ya kudumisha amani ili kuweza kufanikisha malengo yaliyowekwa na mashirika mbalimbali ya kijamii yanafadhiriwa na shirika la Forum CIV hapa jimboni Marsabit.

Kwa upande wake mshirikishi wa shirika la Initiative for Progressive change (IFPC) Hassan Mulata amesisitiza ushirikiano ambao ameutaja kwamba utawezesha mipangilio iliyowekwa kufaniskisha ajenda hizo kufaulu.

Kauli yake Mulata imeshabikiwa na Tumal Orto ambaye ameitaja haja ya kushirikiana ili kusaka Suluhu la kudumu kwa changamoto zinazoadhiri wanaMarsabit.

Tumal ameyataka mashirika yasiyo ya kiserekali pia kushirikiana na kuhakikisha kwamba ujumbe huo unafika mashinaani.

Subscribe to eNewsletter