Local Bulletins

Marurupu ya wanagenzi (interns) waliohudumu Marsabit mwaka jana ulijumlishwa kwenye bajeti ya zaida uliopitishwa na bunge – Asema MCA

NA SAMUEL KOSGEI

Maslahi ya wanafunzi wa nyanjani (Interns) waliofanya kazi kwenye idara mbali mbali za serikali ya kaunti ya Marsabit 2024 kwenye kandarasi ya mwaka mmoja yametiliwa maanani na kujumlishwa kwenye bajeti ya ziada iliyopitishwa na bunge la Marsabit mwezi jana.

kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Marsabit Daud Tomasot aliyeambia kituo hiki kuwa wanafunzi hao ambao wanadai serikali ya jimbo marupurupu ya miezi mitatu watalipwa kwani kamati yake ilitenga pesa kwa ajili ya wanafunzi hao ambao kandarasi yao ilikamilika September mwaka jana.

Amesema japo bunge katika mwaka wa kifedha wa 2024/25 halikuwatengea fedha zozote kilio chao kilizingatiwa kwenye bajeti ya ziada kwani ipo kwenye orodha ya madeni ya kaunti.

Kwa muda vijana hao wanagenzi wamekuwa wakitoa wito kwa serikali ya kaunti kuwakumbuka na kuwalipa pesa hizo ambazo sasa zimekaa kwa Zaidi ya miezi mitano tangu kandarasi yao ikamilike.

Watu wasiojiweza na walio kwenye umaskini wa hali ya juu kaunti ya Marsabit na haswa walio kwenye mpango HSNP wameendelea kutoa wito kwa serikali kupitia mamlaka ya NDMA kuwapa pesa wanazodai kwa zaidi ya miezi minane.

Mmoja wa wanaonufaika na mpango wa HSNP Abdulahi Mohamed kutoka eneo la Shauri Yako ameambia shajara kuwa pesa hizo ziliwafaa sana wakati zilitolewa kwa muda mwafaka.

Anasema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani hela hizo zingewasaidia sana iwapo zingetolewa.

 

Subscribe to eNewsletter