Local Bulletins

Madaktari wasio na mipaka (MSF) wawasili,Moite kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Surua maarufu Measles.

Na Isaac Waihenya,

Madaktari wasio na mipaka (MSF) wamewasili katika eneo la Moite ili kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Surua maarufu Measles ulioripotiwa kuzuka wiki jana katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa afisa wa afya katika kaunti ndogo ya Laisamis Yusuf Galmogle ni kuwa wataalam hao wa afya waliwasili katika eneo la Moite hiyo jana jioni kwa lengo la kufanya vipo zaidi na kutoa hamasa pia kwa wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu Galmogle amesema kuwa idara ya afya inashirikiana na wataalam hao ili kuhakiksiah kwamba wanaougua ugojwa huo wa sarua wanapata tiba.

Aidha Galmogle ameweka wazi kuwa tayari idara ya afya imepeleka chanjo pamoja na dawa za kutibu maradhi hayo katika eneo la Moite huku wanaougugua maradhi ya Surua wakiendelea kupokea matibabu.

Subscribe to eNewsletter