Local Bulletins

Machifu sasa watafika kwa DCI kuandikisha taarifa iwapo visa vya uhalifu vitafanyika katika kata zao. -Asema Kamishna wa Marsabit James Kamau.

Na Isaac Waihenya,

Jambo likifanyika kwako wewe chifu ndie utawajibika.

Hayo ni kwa mujibu wa kamishina wa kaunti ya Marsabit James Kamau.

Akizungumza wakati wa mkao uliowaleta pamoja viongozi wa kijamii katika kaunti ya Marsabit, kamishina Kamau ametaja kwamba kwa sasa hakuna chifu atakayesazwa iwapo maswala ya ukosefu wa usalama yatatokea katika kata yake.

Hata hivyo mkuu huyu wa usalama jimboni amewataka machifu kuwajibika na kuhakikisha kwamba wanapata taarifa kuwahusu wahalifu wanaotekeleza maovu mashinani.

Amesema kuwa machifu sasa watafikishwa kwa DCI kuandikisha taarifa.Kamishina Kamau amewataka machifu kuwasilisha orodha ya wahalifu wote vijijini mwao kwa DCC ili kufanikisha uchunguzi wa visa vya uhalifu.

Kadhalika kamishina Kamau amewataka wazee na viongozi wa kidini kushirikiana na machifu ili kufanikisha hilo.

Subscribe to eNewsletter