Local Bulletins

Maafisaa wa NACADA wakamata zaidi ya katoni 180 za pombe haramu katika kaunti ya Marsabit

Na Joseph Muchai

Maafisa wa NACADA kwa ushirikiano na maafisa wa polisi, mamlaka ya kukadiria ubora wa bidhaa KEBS na mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA wamekamata katoni 189 isiyo na nembo katika oparesheni dhidi ya pombe haramu katika kaunti ya Marsabit.

Akiongea na wanahabari mratibu wa ukanda wa mashariki ya juu Bi Alice Mwangi amesema kuwa zoezi hilo ambalo limeingia siku yake ya pili limefanikisha kukamatwa kwa wanabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa pombe zisizo halali.

Amesema kuwa zoezi hilo linalenga maeneo yote yaliomo katika kaunti ya Marsabit. Aidha amewataka watumiaji wa pombe kuwa macho ili kujiepusha na bidhaa zinazoweza kuwaletea madhara.

Kwa upande wake msimamizi wa KRA  katika oparesheni hiyo Mohamed Musa ameomba jami kuhakikisha kuwa wanajiepusha na pombe zisizo na nembo maana huenda zikawa hatari  kwa afya zao.

Kulingana na mwakilishi wa NACADA hapa marsabit Fredrick ochieng ushirikiano baina ya jamii na maafisaa wa serikali unahitajika ili kuwe na kufaulu katika vita dhidi ya mihadarati na dawa za kulevya.

Aidha Ochieng ameahidi kuwa vita dhidi ya pombe haramu katika kaunti hii vingali vinaendelea.

Subscribe to eNewsletter