KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Samuel Kosgei
KUNA haja ya serikali ya kitaifa kutimiza ahadi yake ya kutuma pesa za kufadhili masomo ya shule za sekondari ili kurahisisha oparesheni za shule.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KUPPET tawi la Masabit Sarr Galgalo aliyeambia shajara kuwa walimu wakuu wamechoshwa na ahadi hewa ya serikali kuwa watatumiwa pesa za kuendesha oparesheni za shule japo hilo halijatimizwa.
Anasema kuwa hilo limesababisha shule kuumia ikizingatiwa kuwa walimu wakuu wanakosa pesa za kulipa wafanyibiashara wanaotoa huduma kwa shule mbali mbali.
Ameongeza kuwa endapo pesa hizo hazitalipwa kufikia wiki ijayo chama hicho cha KUPPET kitaitisha mgomo wa walimu.
Sarr aidha ameshutumu msimamo wa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili KESSHA nchini uliolalamikia mbinu ilitumiwa na tume ya kuajiri walimu TSC kupandisha vyeo walimu wakuu na manaibu wao nchini.
KESSHA kupitia mwenyekiti wao Willy Kuria alidai kuwa mbinu iliyotumiwa na TSC ilikuwa baguzi kwa eneo lenye walimu wengi na haswa walio na tajriba.
Sarr anasema kuwa TSC ilikuwa sawa kuwapandisha cheo walimu wa maeneo kame pia bila kupendelea sehemu nyingine za nchi.
TSC mwaka jana ilitangaza nafasi 19,943 ya kupandisha walimu vyeo.
Wakati huo Galgalo amewaomba walimu wao waliokosa matibabu kupitia bima inayowahudumia kupeleka malalamishi yao katika ofisi yake ili waweze kufuatilia badala ya kurushia cheche za matusi masharika ya bima husika.