Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Huku wataalamu wa elimu wakipongeza mfumo wa elimu chini ya C.B.C baadhi ya watalaam hao katika kaunti ya Nairobi wamesema kufunza wanafunzi lugha ya kifaransa shuleni ina umuhimu kwani itasaidia katika kuboresha sekta ya biashara , elimu pamoja na mahusiano ya kidiplomasia .
Aidha ,katika kaunti ya marsabit wazazi wametoa maoni yao kulingana na pendekezo hilo la kutaka kuwafunza wanafunzi somo la kifaransa katika elimu mpya ya C.B.C wakidai kuwa cha muhimu ni kuwafunza lugha ambazo zinakuzwa katika taifa letu.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi yao wamesema kuwa cha msingi ni kuendeleza masomo ya C.B.C huku wakikitaka ufafanuzi wa kutosha haswa katika kuenzi masomo ya C.B.C
Wakati huo huo , baadhi yao wamesema kuwa ipo umuhimu wa kufunza wanafunzi hao lugha nyingine na sio tu lugha ya kifaransa ili kukuza utamaduni wao.
Pia baadhi ya wazazi mjini marsabit wamepinga himizo hilo wakisema ni sharti wajumuishe lugha ya mama pamoja na mila katika mfumo wa C.B.C kwani ina manufaa kwa wanafunzi hao..