Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Joseph Muchai,
Kujiondoa kwa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat sio suluhu la kupata haki kwa mauaji ya Mwalimu Albert Ojwang.
Haya ni kwa mujibu wa baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Marsabit.
Wakizungumza na Shjara Ya Radio Jangwani wakaazi hao wanahisi kuwa naibu jenerali wa polisi Eliud Lagat alifaa kujiuzulu iwapp alitaka uchunguzi kufanyika na haki kupatikana.
Hata hiyo baadhi yao wanahisi kuwa haki ya Ojwang imeanza kuonesha dalili za kupatikana wakihoji kuwa kujiondoa kwa Lagat ni hatua ya kwanza muhimu ya kupatika na kwa haki.
Wakati uo huo wengine wao wameonesha kutamaushwa kwao na hali ya sasa ya idara ya usalama wakipendekeza kujiondoa kwa waziri wa maswala ya ndani Kipchumba Murkomen, inspekta mkuu wa polisi Doughlas Kanja na manaibu wake wawili kutokana na wanachosema ni kukosa uadilifu kazini.
Pia baadhi wanapendekeza kuvunjiliwa mbali kwa huduma ya kitaifa ya polisi nchini NPS swala liliopingwa na wengine.
Haya yanajiri muda mfupi baada ya babake marehemu Ojwang, Meshak Ojwang kutishia kujiunga na Wakenya wengine kwenye maandamano ya kutafuta haki ya mwanawe iwapo itacheleweshwa. Albert Ojwang aliuawa katika seli za kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi swala ambalo limezua kizazaa humu nchini wengi wakihoji utendakazi wa polisi.