KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Wizara ya elimu katika kaunti ya Marsabit imewataka wazazi wa wanafunzi wanaofadhiliwa na serekali ya kaunti ya Marsabit kuwa na subira ili kuruhusu kesi iliyowasilishwa mahakamani kuhusiana na ufadhili huo kukamilika.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu waziri wa elimu katika kaunti ya Marsabit Ambaro Abdullahi amesema kuwa kwa sasa serekali ya kaunti haiwezi kutuma fedha katika shule mbalimbali kutokana na kesi hiyo inayowazuia kufanya vile.
Waziri Ambaro ametaja kwamba punde tu kesi hiyo itakapokalika mnamo tarehe 24 mwezi ujao basi serekali ya kaunti itaendeleza majukumu yake ya kulipa karo kwa wanafunzi wote.
Amesema kuwa kwa sasa idara ya elimu imewandikia barua walimu wakuu wote katika shule ambazo kuna wanafunzi wanaofadhiliwa na serekali ya kaunti kwamba wawe na subira na kutowatuma wanafunzi nyumbani hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Kuhusiana na swala la shule msingi ya El Molo iliyoko eneo la Loiyangalani, waziri Ambaro amesema kuwa mikakati imewekwa kuhakikisha kwamba shule hiyo inahamishwa hadi eneo salama baada ya baadhi ya madarasa kuharibiwa na maji kutoka na kufura kwa ziwa Turkana.