Local Bulletins

Kaunti ya Marsabit yatajwa kuwa bingwa wa mtihani wa KCSE 2024 ukanda wa Mashariki

NA JB NATELENG

Kaunti ya Marsabit ndio mabingwa wa mtihani wa kitaifa wa KCSE 2024 kanda ya mashariki.

Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu kaunti hiyo Peter Magiri.

Akizungunga alipokuwa akizindua rasmi mashindano ya muhula wa kwanza kwa shule za upili kaunti ya Marsabit, iliyofanyika katika shule ya upili ya Moi Girls, Magiri amesema kuwa bidi, kujitolea na ushirikiano uliyopo baina ya wanafunzi, walimu, wazazi pamoja na washikadau wa elimu jimboni ndio chanzo cha ubingwa huu.

Magiri ameelezea kuwa kaunti ya Marsabit inazidi kupiga hatua kwa masuala ya elimu na ukuzaji wa vipaji.

Mkurugenzi huyu amewarai wanafunzi kuweza kutumia mashindano hayo kuonyesha na kukuza talanta zao akiahidi kuwa ataandamana na timu ambayo itashinda kuelekea mashindano ya mkoa wiki ijayo.

Mashindano hayo yanayaoendelea na ambayo yanatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi inajumuisha shule zote zilizohitimu katika mashindano ya kaunti ndogo yaliyofanyika mwezi jana huku watakaoshinda kwenye mashindano hayo wiki hii wakitarajiwa kuenda hatua ya mkoa wiki ijayo.

Mashindano haya yanajumuisha riadha, mpira wa mkono(handball), mpira wa kikapu (Basketball), kurusha mkuki, kuruka na raga kwa wanaume pekee.

Subscribe to eNewsletter