Local Bulletins

Kampuni ya Lake Turkana Wind Power yalaumiwa kwa kutoziba mashimo katika kijiji cha Sarima na kupelekea kifo cha mtoto wa miaka 6.

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi wa eneo la Sarima wadi ya Loiyangalani katika eneo bunge la Laisamis kauti ya Marsabit, wamelalamikia kile wamekitaja kwamba ni maapuza kutoka kwa shirika la Lake Turkana Wind Power yaliyopelekea mtoto wa miaka 6 kufariki baada ya kuanguka kwenye shilo lililokuwa limejaa maji.

Wakizungumza na idhaa hii kupitia njia ya simu wakaazi hao wakiongozwa na mzee wa kijiji Simom Ekitoe wamesema kuwa licha ya wao kulalamikia kampuni hiyo kuziba mashimo ambayo yamo kijijini baada ya kuchimba mchanga, kampuni hiyo haijafanya vile.

Kauli yao inajiri baada ya mtoto wa miaka 6 kuanguka katika shimo moja lililojaa maji alipokuwa akichunga mbuzi mnamo saa kumi na moja jioni siku ya Jumamosi tarehe 10 mwezi huu wa mei na kuaga duania, huku mwili wake ukiopolewa hapo jana asubuhi na kisha akazikwa jana jioni.

Kando na hilo wakaazi hao wametaja kwamba wamekadiria hasara kubwa kutokana na utepetevu wa kampuni ya Lake Turkana Wind Power kutoziba mashimo hayo kwani wamepoteza pia mifugo wao huku wengine wakipata majeraha.

Subscribe to eNewsletter