Local Bulletins

Kampuni ya kutoa huduma za maji kaunti ya Marsabit MARWASCO kufikia wateja wengi licha ya mfadhili kujiondoa.

Na Samuel Kosgei

KAMPUNI ya kutoa huduma za maji na majitaka kaunti ya Marsabit MARWASCO imesema kuwa kampuni hiyo imepiga hatua kubwa katika shughuli ya kuunganisha mifereji ya maji katika sehemu mbalimbali mjini Marsabit licha ya mfadhili kujiondoa.

Afisa anayesimamia oparesheni na huduma na urekebishaji katika kampuni hiyo, John Halkano ameambia shajara kuwa tayari kampuni hiyo imeunganisha sehemu nyingi za Marsabit mjini na mifereji mpya ili kufanikisha usambazaji wa maji.

Anasema kuwa wateja 125 wamesaka huduma zao za kuwekewa maji na tayari wateja 34 wameunganishwa.

Licha ya kujiondoa kwa shirika la USAID kupitia mradi wa ustawi mashinani anasema kuwa kampuni yao itaendeleza huduma hizo kupitia msaada wa serikali ya kaunti ya Marsabit.

Aidha anasema kuwa licha ya viwango vya maji kushuka katika bwawa la Bakuli iliyo Mlima Marsabit anasema kuwa maji hayo yana uwezo wa kutumikia wananchi wa mji wa Marsabit kwa Zaidi ya miezi mitatu.

Subscribe to eNewsletter