Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng,
Jamii imetakiwa kuwapokea waathiriwa wa dhulma za kijinsia na kuwaonyesha upendo.
Haya ni kwa mujibu wa Mtawa Mourine kutoka shirika la st Teresa Charity Sisters jimboni Marsabit.
Mtawa Mourine ameelezea kuwa kumekuwa na visa ambapo wanajamii wanakataa kumpokea waathiriwa wa dhulma za kijinsia baada ya kunusuriwa na kupewa mafunzo imara ili kuwasaidia katika maisha yao ya baadae.
Mtawa Mourine amekashifu mila potovu ambayo inawafananisha waathirika kuwa watu wasio na hadhi katika jamii huku akiitaka jamii kuweza kuasi mila hiyo na kuwakumbatia waathiriwa hawa.
Mtawa Mourine hata hivo ameelezea kuwa bado visa vya mimba na ndoa za mapema vinazidi kuripotiwa katika kaunti ya Marsabit huku akitoa wito kwa serekali kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserekali ili kutokomeza visa hivi.