Local Bulletins

Jamii ya Marsabit yatakiwa kukumbani mbinu mbadala za maisha kuliko kutegemea tu ufugaji pekee…

Na Isaac Waihenya,

Jamii ya Marsabit imetakiwa kukumbani mbinu mbadala za maisha kuliko kutegemea tu ufugaji ambao kwa asilimia kubwa umeadhirika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamekaririwa na mshikishi wa shirika la Friends of lake Turkana Makambo Lotorobo.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mafunzo ya siku tatu ya wanachama wa kamati za mabadiliko ya tabia nchi kutoka wadi mbalimbali za katika kaunti ya Marsabit yaliyoandaliwa hapa mjini Marsabit, Makambo amesema kwamba ipo hoja ya wanachama wa kamati za mabadiliko ya tabia nchi kupigwa jeki ili kuweza kuhakikisha kwamba wanafanya kazi yao ipasavyo.

Aidha Makambo ameweka wazi kuwa katika mafunzo hayo imejitokeza kwamaba wanachama hao wanahitaji kupewa hamasa zaidi sawa na kuwepo kwa ushirikiano na washikadau pamoja na mashirika mengine jimboni ili kufakikisha vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mafunzo hayo wamelipongeza shirika la Friends of Lake Turkana huku wakiahidi kuwa mabalozi wema mashinani katika kueneza ujumbe utakaosaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.

Subscribe to eNewsletter