Local Bulletins

Jamii ya Marsabit yahimizwa kuwachagua wanawake kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali.

Na JB Nateleng,

Ipo haja ya kutoa hamasa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwachagua wanawake kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali jimboni Marsabit.

Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la MWADO, Mwanaharakati Nuria Gollo.

Nuria aliyezungumza na meza yetu ya habari kwa njia ya kipekee amesema kuwa bado jamii haijaenzi uongozi wa wanawake akitaja kisa cha kutimuliwa kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza kuwa ni dhihirisho tosha ya jinsi uongozi wa wanawake haujapewa kipaumbele kwenye ulingo wa kisiasa.

Aidha Nuria ameelezea kuwa hatua ya Mwangaza Kung`atuliwa mamlakani imewaponza sana akina mama huku akizitaka jamii zote nchini kuchukua suala hili kwa uzito ili kuleta usawa kwenye ulingo wa siasa.

Mwanaharakati huyu amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kwa wanasiasa wa kike wanaposaka uungwaji mkono kwa sababu wenzao wa kiume hutumia mbinu mbalimbali kuwadunisha na kufanya jamii kuamini kuwa uongozi wa wanawake haufai.

Nuria amewachangamoto wakazi wa Marsabit kuweza kukumbatia uongozi wa wanawake akisema kuwa wanawake ni watu wa maendeleo.

Subscribe to eNewsletter