Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Isaac Waihenya,
Vijana waliokuwa wameajiriwa kama wanafunzi wa nyanjani maarufu Interns katika idara mbalimbali za serekali ya kaunti ya Marsabit kuanzi Septemba 2023 hadi Agosti 2024, wamelalamikia kile wamekitaja kwamba ni serekali ya kaunti ya Marsabit kukataa kuwalipa misharara yao iliyosalia baada ya kupindi chao cha kuhudumu kukamilika.
Kwenye ujumbe uliotumwa kwa vyombo vya habari, wanafunzi hao wa nyanjani zaidi ya 700 saba wamelalama kuwa idara ya fedha katika kaunti ya Marsabit imepuuza kilio chao licha ya wao kukamilisha mikataba yao miezi 8 iliyopita.
Wanasema kuwa baadhi yao hawajalipwa deni la mishahara ya miezi mitano huku wengine wakidai mshahara wa miezi mitatu baada ya kupokea malipo ya miezi 7 na miezi 9 mtawalia.
Hata hivyo wameitaka idara husika pamoja na gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamed Ali kuingila kati ili kuhakikisha kwamba wanapata haki yao.