Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Henry Khoyan,
Msemaji wa serikali katika kaunti ya Marsabit, Abdub Barille, ametangaza kwamba vijana waliokuwa wameajiriwa kama wanafunzi wa nyanjani (interns) huenda watalipwa marupurupu yao wiki ijayo.
Barille amesisitiza dhamira ya serikali ya kaunti kuhakikisha kuwa haki ya vijana inaheshimiwa na kwamba malipo yao yanatolewa bila kuchelewa.
Katika taarifa yake, Barille amesema kuwa mtendaji wa bajeti alikumbwa na changamoto ya kushughulikia suala hilo kwa wakati, hali iliyopelekea kucheleweshwa kwa utoaji wa fedha hizo.
Ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi wa bajeti kuimarisha ushirikiano na wadau wengine, ili kuhakikisha kwamba masuala kama haya yanashughulikiwa kwa ufanisi na kwa wakati.
Kulingana na Barille, ni kuwa wanafunzi hao wa nyanjani watalipwa marupurupu yao yote wanayodai serekali ya kaunti.