KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Idara ya vijana na michezo katika kaunti ya Marsabit inaanda mafunzo ya siku mbili kwa vijana kuhusiana na jinsi ya kupata bima ili kutunza biashara zao, afya au hata bodaboda zao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambayo yanafanywa na mamlaka ya udhibiti wa bima nchini (IRA) naibu mkurugenzi katika idara ya vijana na michezo katika kaunti ya Marsabit Galgallo Sarr amesema kuwa mafunzo haya yanalenga kuimarisha biashara za vijana wa jimbo la Marsabit na kuwazuia na hasara zinazoweza epukika.
Aidha Sarr amewataka vijana kuhakikisha kwamba biashara zao na vifaa vyao vinabima ili kuhakisha kwamba mikasa kama ya moto au wizi haiwarudishi nyuma katika hatua za kujiinua ambazo tayari wamepiga.
Hata hivyo Sarr amewarai vijana kujisajili na shirikisho la soka FKF ili kuweza kushiriki kwenye michuano ya kabumbu inayotarajiwa kuong’oa nanga mwaka huu.