Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Samuel Kosgei
HUENDA hali ya lishe kwa mfugo ikiwa mbaya iwapo mvua haitanyesha katika sehemu nyingi za kaunti ndogo ya North Horr, Marsabit.
Hayo ni kulingana na naibu kamishna wa North Horr Tobias Okoth aliyeambia kituo hiki kuwa kwa sasa bado nyasi za mifugo zipo ila huenda zikaisha iwapo mvua zitachelewa kunyesha.
Anasema pia kuwa serikali ya taifa inajibidiisha kuwapa wananchi msaada wa chakula kwa sasa ili kuwakinga dhidi ya makali ya njaa ambayo mara nyingi huathiri sehemu hizo.
Zaidi ya hayo mkuu huyo wa usalama North Horr ameitaka jamii zinazoishi eneo hilo kuzidi kuishi kwa amani na kushirikiana na majirani wao ili kufanikisha ajenda za maendeleo na elimu ya watoto.
Amesema kwa sasa idara yake inaendesha mikutano ya Amani baina ya jamii, mara hii wakihusisha vijana wanaochunga mifugo Fora.
Aidha DCC Okoth amewataka wazazi North Horr kuhakikisha kuwa wanao wanarudi shule wote haswa wiki hii baada ya kuwa nyumbani kwa likizo fupi.
Amesema hakuna sababu yoyote ambayo itamfanya mzazi kutompeleka mtoto wake shuleni haswa wanaosoma shule za msingi na zile za Junior Secondary.