Serikali ya jimbo la Marsabit latakiwa kuongeza vifaa vya kuzoa takataka mjini na viunga vyake.
June 17, 2025
Na Caroline Waforo,
Idara ya usalama kaunti ya Marsabit imelaumiwa kwa utepetevu katika kusuluhisha visa vya wizi wa bodaboda hapa mjini Marsabit.
Idara hii sasa imetakiwa kuwajibika katika majukumu yake na hata kuhakikisha kuwa haki inapatikana kufuatia mauaji ya mhudumu moja wa bodaboda viungani mwa mji wa Marsabit.
Wakizungumza wakati wa mkutano kati ya idara ya usalama na wahudumu wa bodaboda ulioadaliwa hapo jana hapa mjini Marsabit wahudumu hao wamelaumu vikali idara hiyo kwa kile wanasema ni kutochukulia na uzito visa vya wizi wa bodaboda humu mjini.
Kwa upande wake naibu kamishna wa Marsabit Central David Saruni aliyezungumza na Shajara Ya Radio Jangwani leo hii amesema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini kiini cha mauji hayo.
Saruni hata hivyo amewashauri wamiliki wa bodaboda Marsabit wakishauriwa kuweka vifaa ya uangalizi wa bodaboda yaani trackers ili kuzuia visa vya wizi wa bodaboda.
Amedokeza kuwa hiyo inakuwa namna moja ya wahudumu hao kuchukua tahadhari.
Wahudumu hao pia wametakiwa kuboresha uongozi wa bodaboda katika kila steji ili kuimarisha shughuli zao huku wakitakiwa kuchukua tahadhari wakati ambapo wanaendelea na shughuli zao za kila siku.
Vile vile wahudumu hao wametakiwa kutoa taarifa muhimu kwa idara ya usalama naibu kamishna Saruni akisema kuwa wameweka mikakati ya kuwahakikisha kuna usiri wakati wa kutoa taarifa hiyo.
Mkutano huo uliandaliwa kufuatia maandamano yaliyofanyika siku ya Jumanne baada ya mhudumu moja wa bodaboda kuuawa kinyama kwa kudungwa visu mara kadhaa katika eneo la Arobota lililoko nje kidogo ya mji wa Marsabit.