Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia idara ya usajili wa watu imekana madai kuwa raia wasio wakenya wanapewa vitambulisho vya taifa.
Akizungumza na radio jangwani, mkuu wa ofisi ya usajili wa raia kaunti ya Marsabit Isaac Kibet, amesema kuwa hatua zote za kisheria zinafuatwa na wakuu wote wa usajili wa watu katika kaunti ndogo zote za Marsabit. Anasema ofisi yake ikishirikiana na machifu inadhibitisha stakabadhi na asilia ya mtu yeyote yule kabla ya kupewa kitambulisho cha kitaifa.
Hata hivyo amesema kuwa pindi panapokuwa na shauku au tashwishwi yoyote, ofisi yake huomba usaidizi kupitia idara yay a DCI na ile ya ujasusi NIS ili kuondoa wasiwasi itakapojiri.
Wakati uo huo amewataka maafisa wa idara hiyo katika kaunti ndogo kufuata sheria inavyosema wakati wa mchakato wa kutoa kitambulisho.
Aidha amesema kuwa bado watu wengi katika kaunti ya Marsabit wanajitokeza kujisajili kupata vitambulisho ishara kwamba kikwazo cha kupiga msasa kilifungia wengi njia za kupata kitambulisho cha kitaifa.
Anasema lengo lao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anayefuzu kupata kitambulisho anapokezwa kama amri ya rais ilivyosema.