Local Bulletins

Idara ya afya Marsabit yatakiwa kufanya vipimo na kuchunguza hali ya ugonjwa unaohofiwa kuwa ni ugonjwa wa Kalazaar.

Na Isaac Waihenya & JB Nateleng,

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Moite, Samuel Amuroe ameitaka idara ya afya katika kaunti ya Marsabit kufika eneo hilo ili kufanya vipimo na kuchunguza hali ya ugonjwa wanaohofia kuwa huenda ukawa ni ugonjwa wa Kalazaar.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu,Amuroe amesema kuwa zaidi ya wanafunzi 20 wanaonyesha dalili sawa na mmoja wa wanafunzi hao ambae kwa sasa amelaza katika hospitali ya Lodwar baada yake kugunduliwa na ugonjwa wa Kalazaar wiki jana.

Mwalimu Amuroe ameitaka idara ya afya jimboni Marsabit kuharakisha juhudi za kimatibabu katika eneo hilo kwani huenda hali hiyo ikipita viwango iwapo haitaangaziwa mapema iwezekanavyo.

Amesema kuwa hilo linaadhiri pia elimu ya watoto wa eneo hilo.

Kwa upande wake waziri wa afya jimboni Marsabit Malicha Boru ni kwamba maafisa wa afya bado wanazidi kufanya uchunguzi katika eneo hilo ili kusaidia katika kutambua aina ya ugonjwa unaoadhiri watoto na kutoa suluhu inayofaa.

Waziri Malicha ambaye pia alizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu amesema kuwa kufikia sasa hali ya ugonjwa wa Kalazaar umedhibitiwa ipasavyo huku serekali imechukua hatua za kunyunyizia dawa maeneo ambayo yalikuwa yameadhirika na ugonjwa huo.

Kadhalika waziri Malicha amesema kuwa idara ya afya jimboni imejipanga na vifaa pamoja na dawa ambazo zitasaidia katika kupambana na hali hiyo.

Subscribe to eNewsletter