Local Bulletins

Idadi kubwa ya wanaume ndio huathirika zaidi na ugonjwa wa figo kuliko wanawake katika jimbo kaunti ya Marsabit.

Na JB Nateleng

Wanaume ndio huadhirika Zaidi na ugonjwa wa figo kuliko wanawake katika jimbo la Marsabit.

Haya yamebainika katika sherehe ya kuadhimisha siku ya figo duniani iliyoadhimishwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.

Kwa mujibu wa maafisa wa afya katika kaunti ya Marsabit ni kwamba Wanaume wanatabia ya kupuuzilia matibabu ya mapema huku wengi wao wakienda hospitalini kusaka matibabu wakati ugonjwa huo umewadhuru.

Hata hivyo afisa mkuu katika idara ya afya Daktari Halkano Arero amesema kwamba ni sharti kila mmoja kubadili mtindo wa maisha kwa kuangazia lishe yao ili kupunguza visa hivi vya ugonjwa huu wa figo.

Kauli yake Arero imeungwa mkono na afisa mkuu katika idara ya afya ya umma Omar Boku ambaye amesema kuwa hatua ya kwanza ya kinga inatokana na maamuzi ya mtu binafsi.

Wakati huo huo Waziri wa afya kaunti ya Marsabit Malicha Boru amewataka maafisa wa afya kuweza kutoa hamasa Zaidi kwa vijana kuhusu hatari inayotokana na wao kujiingiza katika matumizi ya mihadarati.

Tarehe 13 machi huwa imetengwa kwa ajili ya kusherehekea siku ya figo duniani. Siku hii huwa inatumika kutoa hamasa kwa jamii kuhusu uhamasishaji wa afya inayozingatia umuhimu wa figo na kupunguza athari zinazokumba figo na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa figo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Je figo zako ziko sawa?, gundua mapema, linda afya ya figo”

Subscribe to eNewsletter