Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Huenda visa vya utapiamlo vikaongezeka pakubwa katika lokesheni ya Hurii Hills iliyoko katika eneo bunge la North Horr kaunti ya Marsabit kufuatia uhaba wa chakula unaoshuhudiwa kwa sasa kutokana na kiangazi kinachoshuhudiwa jimboni.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema kuwa wanaikodolea macho hatari kutokana na uhaba huo wa maji na chakula.
Wakizungumza na wanahabari Leo Jumanne katika kikao cha kutoa hamasa kuhusiana na umuhimu wa jamii kutoa ardhi kwa ajili ya miradi ya kuhifadhi mazingira, kikao kilichoongozwa na idara ya misitu jimboni, wakaazi hao wakiongozwa na mhudumu moja wa afya wa kujitolea CHP Mohammed Shariff wanasema kuwa watoto wadogo pamoja na wanawake wajawazito tayari wameanza kuonyesha dalili za hali ya utapiamlo.
Mzee Guyo Ibrae Jillo na ambaye amesisitiza madhira yanayowakumba kutokana na kiangazi amesema kuwa hapo awali waliomba msaada wa serikali ila hawakupata sasa wakiitaka serikali kuwapa msaada wa dharura.
Akiwakilisha vijana katika eneo hilo Hassan amesema kuwa jamii inatatizika pakubwa kutokana na uhaba wa maji wakilazimika kusafiri masafa marefu ili kusaka maji ya matumizi ya kinyumbani
Hassan anadai kuwa kutokana na hilo baadhi ya wakaazi wameyahama makwao katika juhudi za kukwepa madhila haya.
Kulingana na wakaazi hao shule pia zimeathirika kwa kiasi kikubwa huku sasa wakihofia huenda hali hii ikasababisha wanafunzi kukosa kuhudhuria masomo.
Haya yanajiri huku mamlaka ya kutathmini hali ya ukame nchini NDMA ikisema kuwa wananchi milioni 2.15 kutoka maeneo kame nchini wanakabiliwa na uhaba wa chakula na wanahitaji misaada ya kibinadamu.
Kaunti zinazoathirika pakubwa na kaunti ya Marsabit Turkana, Mandera, Garissa, Wajir