Local Bulletins

Hatujamkamata yeyote kuhusiana na mauaji ya mhudumu wa bodaboda eneo la Harobota,Marsabit. – Asema Kamishna James Kamau.

Na Caroline Waforo,

Hakuna mtu amekamatwa kuhusiana na mauaji ya mhudumu wa bodaboda hivi maajuzi katika eneo la Harobota vyungania vya mji wa Marsabit.

Haya ni kulingana na Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau ambaye amezungumza na Shajara ya Radio Jangwani afisi mwake.

Kamau amesema kuwa uchunguzi unaendelea huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa muhimu kwa idara ya usalama zitakazo saidia katika uchunguzi unaoendelea.

Kadhalika Kamishna Kamau ametoa onyo kali kwa watu wanaowasaidia wahamiaji kuingia humu nchini akisema kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Amedokeza kuwa wameimarisha doria mpakani.

Tarehe 15 mwezi Machi wahamiaji haramu 30 kutoka nchini Eritrea walikamatwa katika eneo la Illeret eneo bunge la Northhorr wakiwa safarini kuelekea jijini Nairobi.

Subscribe to eNewsletter