Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC tawi la Marsabit imedhibitisha kuwa aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya Maikona Madina Marme,amechukua mikoba ya kuiongoza shule ya El-Mosaretu Girls iliyoko wadi ya Loiyangalani katika wadhifa wa mwalimu mkuu.
Akizungumza ns meza ya habari ya Radio Jangwani ofisini mwake mkurugenzi wa TSC tawi la Marsabit Ali Hussein Abdi amedhitisha hilo akitaja kwamba zoezi hilo lilifanyika mnamo siku ya jumatatu wiki hii na kusimamiwa na wawakilishi kutoka katika ofisi yake (TSC) na ile ya mkurugenzi wa elimu jimboni Marsabit Peter Magiri.
Hussein amesema kuwa kwa sasa shughuli za masomo zinaendelea vyema katika shule hiyo.
Aidha Hussein ametaja kwamba ofisi yake haijapokea malalamishi yeyote kutoka kwa wazazi kuhusiana na mwalimu huyo kama inavyodaiwa.
Itakumbukwa kuwa mapema wiki hii wazazi wa shule hiyo ya upili ya wasichana walipinga hatua ya TSC kumhamishia mwalimu huyo shuleni humo.
Wazazi hao walielezea kutofurahishwa kwao na maamuzi ya kumhamisha hadi shule humo mwalimu huyo, ambaye pia alikataliwa na wazazi wa shule ya upili ya Sasura girls mwezi jana wakisema kuwa hawakuridhishwa na maamuzi hayo ya TSC.