Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Samuel Kosgei
GAVANA wa Marsabit Mohamud Ali anaitaka serikali ya kitaifa kuharakisha ujenzi wa barabara ya kuanzia Marsabit mjini hadi Songa ili kufanikisha suala la usalama katika barabara hiyo ambayo kwa muda imekuwa na mavamizi ya majangili.
Gavana Ali akizungumza kwenye mkao wa usalama ulioandaliwa mji Marsabit na kuhudhuriwa na waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, alisema kuwa kwa muda ahadi nyingi zimetolewa siku za nyuma kufanikisha ujenzi wa barabara hiyo ila imesalia kuwa ndoto .
Gavana aidha amemtaka waziri kumkumbusha rais kutimiza ahadi ya kununulia wafugaji wa Marsabit waliopoteza mifugo wakati wa ukame ulioshuhudiwa miaka kadha iliyopita ambapo mifugo mingi ilikufa.
Wakati uo huo amesisitiza haja ya wakaazi wa Marsabit wasio na vitambulisho kutumia fursa hii kusaka vitambulisho vya kitaifa kwani hakuna malipo kwa wote wanaosaka kitambulisho kwa mara ya kwanza.