KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
NA SABALUA MOSES
Gavana wa Marsabit Mohamud Ali ameshutumu visa vya mauaji ya kiholela vilivyofanyika kaunti hii ya Marsabit mwezi huu ambapo kijana mmoja wa bodaboda na wengine wawili kuuliwa katika eneo la Dukana eneobunge la north horr wiki jana na hapo juzi na watu wasiojulikana.
Akizungumza hii leo gavana ali ameonesha masikitiko yake huku akitaka idara ya usalama kuzidisha doria na kuwakamata waliotenda mauaji hayo.
Wakati uo huo Abshiro amewataka walioathirika na misiba hiyo wasilipize kisasi bali waachie idara ya usalama ichukue hatua za kisheria. Ameahidi kuwa ofisi yake itashirikiana na idara ya usalama katika harakati za kuhubiri Amani na usalama.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amewataka wakaazi kudumisha Amani na kushirikiana pamoja katika kuimarisha usalama.
Aidha Kamau amekashifu mauaji ya kiholela akiwataka vijana kuripoti na kutoa habari kwa idara ya usalama ili kuimarisha usalama na kukamata wahalifu wanaohangaisha raia katika kaunti ya Marsabit.