Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Carol Waforo
Eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit ndilo lililoathirika zaidi na kiangazi pamoja na mafuriko.
Idadi kubwa ya wakaazi katika eneo hilo bado wanahitaji misaada ya kiutu na sasa wanaitaka serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kuzindua miradi itakayowawezesha katika kurejelea maisha yao kabla ya majanga.
Wakizungumza katika warsha ya utathmini wa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa usalama wa chakula mashinani iliyoandaliwa na shirika la Christian Aid Kenya kwa ushirikiano na shirika la PACIDA, pamoja na mashirika mengine, waathiriwa hao wamesema kuwa wengi wa wakaazi wametumbukia katika umaskini wa hali ya juu baada ya kupoteza mifugo yao kutokana na kiangazi.
Abdub Qampicha kutoka eneo la North Horr anasema kuwa licha ya misaada inayotolewa kwa sasa bado ipo haja kuu ya wakaazi hao kupokea misaada zaidi.
Abdub ameyataka mashirika hayo kuwanunulia wafugaji mifugo ili kurejelea maisha yao kama kawaida.
Naye Talaso Shano amesema kuwa wakaazi sasa wamelazimika kutegemea fedha za misaada zinazotolewa na mashirika mbalimbali.
Kulingana na afisa mkuu wa mipango katika shirika la PACIDA Galma Qampise Galgallo ni kuwa wameanzisha miradi ya kuwasaidia wafugaji walioathirikana na matatizo ya kisaikolojia kufuatia majanga.
Naye mkuu wa mipango katika shirika la Christian Aid Kenya Jude Otogo amesema kuwa madhumuni ya shirika hilo ni kukabiliana na sababu kuu za umaskini katika jamii, mizozo kati ya maswala mengine.
Otogo amehoji kuwa wengi wa wakaazi katika eneo hilo wamepoteza kitega uchumu kutokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi jambo linalowafanya wakaazi kutegemea misaada ya kiutu.
Kaunti ya Marsabit ni mojawapo ya kaunti ambazo imeathirika pakubwa na mabadiliko ya tabianchi.