Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
NA JB Nateleng
Kuna haja ya kutoa hamasa kwa wanafunzi kuhusu kozi watakazozifanya wanapojiunga na vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaobadili ama kuacha kuacha kozi walizoteuliwa kusomea katika vyuo vikuu.
Haya ni kwa mujibu wa Mwalimu Mark Murugu ambaye ni mkufunzi kutoka chuo kikuu cha Tharaka.
Akizungumza na idhaa hii, kwenye hafla ya kutoa hamasa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne, iliyoandaliwa katika shule ya upili ya Marsabit Mix eneo la Saku kaunti ya Marsabit, Murugu ameelezea kwamba wanafunzi kutoka kaunti ya Marsabit wanaufahamu mchache kuhusu kozi bora ambazo zitawaboresha kitaaluma akisema kuwa jambo hili linafaa kushughulikiwa kwa haraka ili kusaidia kuboresha taswira ya jamii kupitia masomo na kozi zinazofaa.
Murugu amesisitiza kwamba ni sharti hamasa ianze kutolewa kwa wanafunzi pindi tu wanapojiunga na shule za upili ili kujenga msingi imara na dhabiti juu ya kozi zinazofaa.
Aidha Murugu amewataka wazazi kuwaongoza watoto wao katika njia inayofaa ya kuchagua kozi bora badala ya kuwalazimisha kufanya kozi ambazo haziendani na uelewa wao.
Kwa upande wa wanafunzi walioudhuria kikao hicho, wametaja kusaidika na kuwataka wenzao kuweza kujitokeza ili kupata usaidizi unaofaa kuhusiana na kozi bora wanzofaa kusomea.
Chuo kikuu cha Tharaka kimekita kambi katika kaunti ya Marsabit ili kutoa hamasa kwa wanafunzi kuhusu kozi wanazofaa kusomea katika chou kikuu. Hamasa hii ambayo imeanza leo itaendea hadi hapo kesho Jumanne. Katika eneo la Saku hafla hii inafanyika katika shule ya upili ya Dakabaricha na Marsabit Mix.