Local Bulletins

Chifu Enock Kallo aunga mkono pendekezo la waziri Murkomen la Machifu kupewa bunduki.

Caroline Waforo,

Pendekezo la waziri wa Usalama wa ndani Kipchumba Murkomen la machifu walio katika maeneo hatari kupewa bunduki ili kujilinda linaendelea kupongezwa haswa na machifu.

Wa hivi punde ni chifu wa lokesheni ya Jirime Chifu Enock Kallo ambae ameunga mkono mpango huo akisema kwamba utawasaidia kujilinda.

Chifu Kallo ameitaja hatua hiyo kama itakayohakikisha kwamba machifu pia wako salama na kuwaepusha na mashambulizi ambayo huelekezwa kwao kutokana na majukumu yao.

Mpango huo unahusisha machifu kutoka kunti za Marsabit, Isiolo, Meru, Laikipia na  Samburu.

Hii ni baada ya machifu kukiri kuwa wanawafahamu wezi wa mifugo ila wanahofia kuwakamata kutokana na uwoga wa kuvamiwa.

Subscribe to eNewsletter