Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Bodi ya kudhibiti maji nchini WASREB na kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Marsabit MARWASCO zimeandaa kikao cha umaa kutoa maoni kuhusiana na hatua ya kuipa kampuni ya MARWASCO leseni ya miaka 3 ya kuhudumu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo mshirikishi wa bodi ya WASREB David Lelito amesema kwamba hatua hiyo inalenga kuhakikisha kwamba MARWASCO inafanya kazi kulingana na sheria na inatoza ada ambazo zimo katika gazeti rasmi ya serekali.
Aidha Lelito ametetea bei mpya za maji ambazo zimependekezwa na bodi ya WASREB akisema kwamba hilo linalenga kuimarisha huduma na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata bidhaa hiyo muhimu.
Kauli yake imeungwa mkono na mkurugezi wa MARWASCO Sora Katelo ambaye amekariri kuwa kwa sasa kero la kutozwa ada kwa wale hawajumia maji limefika kikomo.
Vilevile Katelo ameweka wazi kuwa kampuni hiyo imeweka mikakati dhabiti kuhakikisha kwamba wananchi wa mashinani wanapata maji pia.
Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Central Jack Elisha amepongeza hatua zilizopigwa na Marwasco akisem akwamba zimetatua kwa asilimia kubwa changamoto za ukosefu wa maji.
Aidhaa baadhi ya wananchi waliozungumza katika kikao hicho wametaja kwamba wameriadhia hatua bodi ya kudhibiti maji nchini WASREB kuipa leseni ya mika mitatu kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Marsabit MARWASCO wakitaja kwamba hilo litaboresha utendakazi wa kampuni hiyo.
Wamepongeza hatua ambazo zimepigwa tangu MARWASCO katika kuhakikisha kwamba wananchi haswa katika wadi ya Marsabit Central wanapata maji.