Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Joseph Muchai,
Askofu wa kanisa la kianglikana jimboni Marsabit Daniel Qampicha amehimiza umuhimu wa amani na maridhiano miongoni mwa jamii zinazoishi hapa jimboni Marsabit.
Akiongea wakati wa utoaji wa vifaa vya ujenzi kwa waathiriwa wa ghasia za mwaka 2022 Qampicha amesema kuwa Amani ni muhimu kwani wakaazi wataweza kujikuza kwenye uwepo wa Amani.
Ameomba serikali na washikadau wengine kujitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa wakaazi wanarejea maisha yao ya kawaida.
Aidha Askofu Qampicha amesema kuwa ijapokuwa wao kama kanisa wamejitolea kuhakikisha kuwa watu wanarejea makwao kumekuwa na changamoto kutokana na uhaba wa fedha kwani watu walioathirika na ghasia hizo ni wengi ambao bado hawajanufaika huku akitoa wito kwa wahisani kuingilia kati na kuwasaidia waathiriwa hao.
Vilevile Kioongozi huyo wa kidini amewataka viongozi kufanya hima na kuwafadhili waathiriwa haswa msimu huu wa mvua.
Kanisa la ACK limekuwa likiwasaidia waathiriwa hao kwa vyakula hifadhi na fedha kwa miezi mitatu sasa.