Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na Isaac Waihenya,
Wakaazi wa eneo la Hurri Hills wamelalamikia kile wamekitaja kwamba ni kutelekezwa na idara ya elimu sawa na hazina ya maenedeleo ya eneo bunge CDF katika eneo bunge la North Horr baada ya upepo kuharibu madarasa mawili katika shule ya msingi ya Shankera mnamo mwezi Januari mwaka huu.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia simu wakaazi hao wakiongozwa na James Barako wametaja kwamba hata licha ya kupiga ripoti kwa idara ya elimu sawa na hazina ya CDF bado mpaka sasa madarasa hayo hayajarekebishwa.
Wakaazi hao wamesema kuwa kwa sasa wanafunzi wanateseka kupata elimu kwani ni madarasa mawili pekee ambayo yamesalia yakiwa katika hali nzuri huku wanafunzi wengine wakilazimika kutumia kanisa lililopo karibu kama darasa.
Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa shule hiyo Yattani Buta Barille ambaye amesisitiza hoja na madarasa hayo kurekebishwa kwani mabati yaliporomoka na hatari kwa maisha na wanafunzi.
Amewarai wahisani kuweza pia kuingilia kati ili kuwasaidia katika kurekebisha madarasa hayo mawili yaliyoharibiw ana upepo kwani ukosefu wa madarasa unaadhiri elimu ya watoto wa eneo hilo.
Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri amekiri kufahamu kuhusuiana na shule hiyo japo ameweka wazi kuwa idara ya elimu haina fedha zozote za kusaidia katika zoezi la kurekebisha shule hiyo.
Magiri hata hivyo amewataka wazazi wa shule hiyo kusaka msaada kutoka kwa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge CDF sawa na wahisani wengile ili kufanikisha zoezi hilo.